Baraka ya Amani
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Walawi 26:6 Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala wala hapana atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu.
Leo ni Siku ya Kusitisha Vita, wakati tunaelekeza mioyo na mawazo yetu kwenye mwisho wa Vita ya Kwanza ya Duniani Yote. Wakati ule, ilisemekana kwamba ile vita ilikuwa vita vya kumaliza vita zote. Lakini mambo hayakutokea kama watu walivyotazamia.
Watu zaidi ya milioni 20 walikufa kwenye Vita ile ya Kwanza ya Dunia Yote. Inatisha kweli lakini tangu pale, ukifuata takwimu zilizo rasmi, kumetokea vita zingine 230, ikiwemwo Vita ya Pili ya Dunia Yote, na kwa jumla watu zaidi ya milioni 70 walikufa kwenye vita zile. Na inawezakana kwamba mahesabu ya kweli yanazidi sana idadi ile.
Aliyeathirika na vita awaye yote, kama vile wazazi wangu, au aliyeishi na mtu ambaye hata sasa hajapona vizuri na kiwewe cha vita, atafahamu jinsi maumivu makali yanaweza kuendelea muda mrefu baada ya mapigano kusitishwa.
Hata kama mimi nilikuwa mwanajeshi, sikuwahi kwenda vitani, kwa hiyo ni rahisi kufikiri kwamba kuwa na amani ni hali ya kawaida. Lakini tusiichukulie hivyo kwa sababu amani ni baraka kubwa kuliko zote zingine ambazo Mungu angetukirimia kwazo. Ndivyo aliwaambia Waisraeli zamani, miaka elfu mbili na nusu iliyopita.
Walawi 26:6 Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala wala hapana atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu.
Sijui kinachoendelea maishani mwako lakini najua hili. Haijalishi ni mgogoro gani unaokumbana nao muda huu, Mungu anataka upokee baraka ya amani yake. Umheshimu kwa hilo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.