... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Bwana Ndiye Akupaye Nguvu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Habakuki 3:19 YEHOVA, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.

Listen to the radio broadcast of

Bwana Ndiye Akupaye Nguvu


Download audio file

Wakati kila jambo linatupinga, wakati mgogoro, kuchanganyikiwa na maumivu vinatushambulia kutoka kila sehemu, kinachohitajika kwetu ni nguvu na wepesi ili tuweze kutokezea upande wa pili.  Hivyo ndivyo vinavyohitajika kweli! 

Jana tuligundua kupitia nabii wa Agano la Kale, Habakuki; kwamba wakati mipango yetu yote mizuri imeharibika, mkakati wa Mungu kutupitisha katika kipindi hicho kigumu ni kutumia imani yenye ujasiri na kumfurahia BWANA na kumshangilia Mungu wa wolovu wetu licha ya dhiki yetu, tukikabiliana nayo kidete. 

Halafu, hata kama haieleweki kikawaida, kwa mstari unaofuata, nabii anatushirikisha kwa mafao ya matukio aliyoyapitia, yaani matokeo ya imani yake yenye ujasiri: 

Habakuki 3:19  YEHOVA, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka. 

Nguvu hizi zinatoka wapi?  Je!  Ni sisi wenyewe tunapaswa kuzitengeneza au?  la!  Bwana Mungu ndiye anipaye nguvu.  Ananipa nguvu kiasi cha kuwezesha miguu yangu kuwa kama ya kulungu, na kuniendesha katika mahali pangu palipoinuka.  

Ebu fikiria jinsi kulungu au swala anavyoweza kuruka juu ya korongo na ufa mkubwa na kufika kwenye usalama wa kilele cha mlima.  Yaani ni dhana halisi ya wepesi na nguvu.  Ni nani alimwezesha Habakuki kufanya hivyo siku yake ya taabu?  Ni Mungu. 

Wakati sisi tunashindwa, Mungu anaweza.  Wakati sisi ni wadhaifu, yeye ni mwenye nguvu halafu ni nguvu na wepesi anataka kuwapatia anaowapenda, hata siku zilizo ngumu kabisa. 

YEHOVA, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy