Bwana Ndiye Akupaye Nguvu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waefeso 3:16,17 Awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo.
Sijui kama umewahi kushuhudia jinsi watu wengine wenye nguvu za kiroho katikati ya dhoruba na tufani za maisha, halafu wengine wanapeperushwa huku na huko kama vile mti unapelekwa na mawimbi ya bahari?
Hizi siku chache, tumeongea habari ya msaada wa Mungu wakati tunajikuta katika kipindi kigumu sana, na havina budi kutokea mara kwa mara. Lakini mara nyingine inatuwia vigumu kuingiza ahadi zake moyoni wakati maisha ni mapambano tu.
Kwa sababu hisia zetu hazitulii muda huo, ni kama zinakuwa kizuizi tusiweze kupokea msaada ambao Mungu alishaandaa kwa ajili yetu. Yamkini ndiyo sababu Mtume Paulo aliomba dua hili kwa ajili ya rafiki zake:
Waefeso 3:16,17 Awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo.
Ni sala ya ajabu kabisa! Na ni sala ninayoiomba leo kwa ajili yako pia; kwamba Mungu afungue madirisha ya mbinguni na kumwaga uwezo wake juu yako ili hata itokee nini, uwe na nguvu katika roho yako. Bila shaka, najua atakupa nguvu zote unazozihitaji wakati atakujaza tele na Roho wake Mtakatifu.
Bwana wetu Yesu Kristo na akae moyoni mwako kwa imani. Akuimarishe na kukutia nguvu katika upendo wake kwa ajili ya utukufu wake!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.