... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Bwana ni Mwaminifu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wathesalonike 3:3 Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.

Listen to the radio broadcast of

Bwana ni Mwaminifu


Download audio file

Jana nilijaribu kueleza kidogo hatua zote za kuandaa kipindi hiki kinacholeta ibada moyoni na namna tunavyokisambaza kila siku duniani kote kwa ajili ya wasikilizaji na watazamaji wetu ma-milioni.

Sielezi hayo ili nijitukuze kwako!?, hapana, tumekosea mara nyingi, Bali fahari yetu ni katika Bwana na yale yote aliyoweza kutenda kupitia Neno Safi na Lenye Afya, hususani yale anayoweza kufanya katika maisha yako. 

2 Wathesalonike 3:3  Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu. 

Lazima mtu ajiulize, Kwanini mstari huu unaanza na neno “Lakini”?  Ni kwa sababu ya yale Mtume Paulo aliyoandika kwenye mstari uliotangulia kuhusu huduma yake ya kutangaza habari njema ya Yesu ulimwengu kote. 

2 Wathesalonike 3:2  Hatimaye, ndugu, tuombeeni … tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.  

Uniamini kwa sababu ninajua kwamba timu yetu ya Neno Safi na Lenye Afya inayoandaa vipindi vyetu vinavyokujia kila siku, wamekumbana na vipingamizi vikali – katika nchi kadhaa wamepata dhiki, majaribu, hatari na mashambuliza ya uadui. 

Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.  

Acha niseme kwa moyo wangu wote, nikakwambia kwamba kweli hii inaweza kuonekana hata katika maisha yako pia.  Haijalishi unakuwa na upinzani wa namna gani, haijalishi uko kwenye mapambano ya namna gani, haijalishi mazingira yako ni magumu kiasi gani Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy