Bwana ni wa Milele
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 90:1,2 Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi. Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
Wewe na mimi, tunaishi maisha ya kila siku tukipambana mara nyingi na mambo madogo madogo. Si vibaya, ndivyo maisha yalivyo. Lakini kuna hatari: tunaweza kuzama katika mambo yale madogo madogo na kutokuona tena yaliyo makubwa na muhimu.
Haya, niambie, je! Leo utafanya nini? Halafu kesho, kesho kutwa? Inawezekana utafanya yale ambayo uliyoyafanya Jumatatu iliyopita, na Jumanne na Jumatano pia. Ndivyo mambo yanavyoenda kawaida. Sasa katika mambo ya kuchosha, inawezekana ikatokea ghafla jambo fulani linaloweza kutugonga bila kutazamiwa na kutupindua kabisa.
Sawa, tunajaribu kukabiliana na tukio lile, tunasimama tena, tunajipangusa vumbi na kuendelea na maisha. Kwa vyo vyote, lazima maisha yaendelee. Halafu siku baada ya siku, macho yetu yanalenga yaliyopo hapa hapa muda huu huu na hii inasababisha furaha yetu, tumaini letu, imani yetu na upendo wetu vipungue kabisa.
Kwa hiyo, leo hii, inua macho yako pamoja nami tutazame yaliyo juu huko mbinguni.
Zaburi 90:1,2 Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi. Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
Safi kabisa! Haleluya! Tangu milele hadi milele daima, Mungu ni Mungu wetu. Alikuwepo, yupo na ataendelea kuwepo milele akiwa makao yetu, kimbilio letu, Mwokozi wetu na furaha yetu.
Mungu wetu ni wa milele tena astahili kusifiwa sana. Je! Anajishughulisha na mambo madogo madogo ya maisha yetu? Je! Anatujali? Jibu ni “Ndiyo kabisa!” Kwa hiyo wakati unaendelea na maisha yako ya kawaida leo, kesho, kesho kutwa … msikilize akiongea tena ukweli huu wa ajabu moyoni wako:
Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.