Cha Kushangaza Mno
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 14:15-17 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Tukizidi kupiga hatua katika mwaka huu mpya, hata kama tuna mashaka, jua kwamba tuko pamoja, tukisafiri mbeleni. Kupitia ujumbe huu wa Neno Safi na Lenye Afya, tunaweza kushikilia neema na uhuru vinavyopatikana sehemu moja tu.
Kadiri mtu anazidi kujuana na watu wengine, ndipo atagundua kwamba kila mtu ana changamoto zake. Halafu dhana ya kukabiliana na mwaka ulio mbele yetu, kwa watu baadhi, inatisha, hususani kwa wale wanaojisikia kuwa peke yao.
Najua kwamba wengi wetu hatuko peke yetu. Mimi nina mke mrembo anayenipenda kwa jinsi isiyoelezeka. Wengine wako kama mimi, wengine hawako hivi. Lakini kwenye kiini cha moyo, pale mtu anapotafakari, katika hisia za ndani mahali nafsi ya mtu inapoishi, bado kuna pengo kubwa ambalo halijajazwa.
Inasemekana kwamba ni pengo saizi ya Mungu mwenyewe, hata kama sisi ni wadogo na Yeye hana mipaka, ni pengo Mungu tu anayoweza kulijaza. Sasa, habari njema, tena ni habari njema mno, ni kwamba Yeye anataka kulijaza na kukamilisha kwa njia ambayo Yeye peke yake awezaye kufanya. Yesu alisema hivi …
Yohana 14:15-17 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Lakini ahadi hii si kwa kila mtu, hapana. Ni kwa wale tu ambao waliamua kumfuata Yesu, kumtii na kutubia maovu yao. Yesu atamwaga Roho yake juu ya mtu kama huyo. Atajaza pengo lile lenye saizi ya Mungu; atamkamilisha kama vile Yeye tu awezaye.
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.