Chombo Kinachomfaa Bwana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 34:17-19 Walilia, naye BWANA akasikia, akawaponya na taabu zao zote. Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka roho huwaokoa. Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini BWANA humponya nayo yote.
Mkono wa Mungu uokoaye ni mada endelevu katika Agano la Kale, hata Agano Jipya. Hii ni habari njema. Habari njema kabisa, kwamba tukipata mateso, Mungu yu nasi ili atuyavushe.
Kama vile mimi, nina hakika kwamba kumekuwa vipindi maishani mwako wakati ulihitaji kuona mkono wa Mungu ukikuokoa, akikutia nguvu na kukutia moyo ili uweze kuvuka kipindi cha hatari. Hata mimi.
Zaburi 34 iliandikwa na Mfalme Daudi wa Israeli akitafakari uaminifu wake Mungu kipindi mojawapo kigumu alichopitia:
Zaburi 34:17-19 Walilia, naye BWANA akasikia, akawaponya na taabu zao zote. Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka roho huwaokoa. Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini BWANA humponya nayo yote.
Maneno hayo ni thibitisho la ajabu kuhusu uaminifu wake Mungu wakati wa mateso na taabu. Anasikia kilio chetu. Anatuponya na taabu zetu zote. Yu karibu nao waliovunjika moyo, na kuwaponya waliopondeka roho.
Haleluya! Lakini unajua, kuna mara anatenda hayo yote kupitia mmoja wa watu wake, kupitia mmoja wetu. Kuna mara anakusudia kujibu, kuokoa, kufariji, kupitia wewe, kupitia mimi.
Je! Uko tayari? Je! Utaenda? Ni fursa kubwa kuwa chombo cha Bwana, chombo kilichoteuliwa tayari kwa kila kazi jema. Lakini usidanganyike. Utagharamiwa. Daima kuna gharama. Tumeitwa tumwige Mungu. Ni jambo jema, ila inabidi ukumbuke kwamba alitufia pale msalabani. Kwa hiyo, acha nikuulize tena, Je! Uko tayari? Je! Utaenda?
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.