Dahana ya msamaha
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waefeso 4:32 Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Ninataka kuwa wazi mbele zenu. Zamani sikuwa mtu mwema hata kidogo. Tangu nilipokuwa kijana, nililenga ushindi na mafanikio, kwa hiyo nilikuwa tayari kukanyaga awaye yeyote, tuseme watu wote, ili nifikie lengo langu. Lakini hatimaye kulitokea mabadiliko. Je! Ni mabadiliko gani? Ni yapi yaliyoniletea mabadiliko makubwa ambayo bado yanaendelea maishani mwangu leo?
Watu ambao niliwavizia zamani ili niwatese walikuwa Wakristo hasa. Walinikwaza mno. Hata kama sikuweza kulitambua wakati ule, wema wao ulinikera kwa sababu ulimulika kusudi langu bovu na mwenendo wangu mbaya.
Sasa baadae miaka ya 1990, wakati mambo yangu yote yaliyoniharibikia kabisa (sina haja kueleza kila kitu, lakini ilikuwa janga kubwa) ni Wakristo wale wale walionifungulia mioyo yao hata nyumba zao. Bila kutamka hata neno moja la kunihukumu, bila kusita-sita, walikuwa karibu nami ili wanisaidie.
Waefeso 4:32 Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Hili ni tendo zuri sana,
Msamaha ule wa wale Wakristo wakati walinisamehe bila kusita wala kuweka masharti ulinigusa sana kuliko mengine, ukinidhihirishia upendo wa Mungu na msamaha wake kwangu kupitia sadaka ya Yesu Kristo pale Msalabani. Kwa hiyo, tafadhali … Iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.