Dakta Livingstone, Eti?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Kutoka 33:13-16 Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; kuakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. Akasesma, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi?
Kama jambo fulani ni la muhimu sana, ni vizuri kulikazia kwa kulitaja mara ya pili, kitu muhimu sana kwako na kwangu na kwa mtu yeyote anayemwamini Yesu.
Musa tayari alikuwa amepitia mengi kwa kuongoza Israeli kutoka utumwani Misri. Kwanza, Farao alituma jeshi lake kuwafuata. Halafu Waisraeli walimteta na kunung’unikia. Kulikuwa na changamoto kuhusu chakula na maji … yaani kila wakati kulitokea shida.
Tulisimulia habari hiyo jana, lakini kama ulinisikiliza, najiuliza, kweli “ulinipata” Kwa tahadhari ninalirudia dua ya Musa aliyomwomba Mungu:
Kutoka 33:13-16 Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; kuakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. Akasesma, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi?
Musa hakutaka kwenda mbele bila Mungu.
Mishionari maarufu wa karne wa 19, David Livingstone, aliomba hivi: Mungu unitume popote pale, ila uende nami. Pia kata mahusiano yote moyoni mwangu kasoro yale yanayoambatanisha moyo wangu na wako.
Hata uwe na safari gani, hata ukitwe kuvuka mipaka gani … usiende peke yako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.