Dhabihu Iliyokubalika Mbele za Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 51:17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
Kwetu ukiona mwanaume anatembea barabarani kashika maua ni aidha kuna mtu anataka kumuonyesha upendo au ni siku kuu fulani … au pengine anataka kumuomba msamaha mpenzi wake aliyemkosea.
Mfano: mume na mke wamezozana. Baadaye mume anajitambua kuwa amekosea, hivyo anapotoka kazini ananunua maua njiani ili ajipatanishe na mke wake tena. Lakini, ni mara ngapi hii inatokea duniani? Nadhani matukio kama hiyo yameingiza ma-bilioni kwenye mapato ya wauza mauwa pamoja na wanaoyalima.
Labda ni desturi inayoshangaza tuliyonayo sisi wazungu, lakini inatokana na dhana ya ki-Mungu kwamba; dhabihu inahitajika kwa kuleta matengenezo, si kweli? Inaashiria dhabihu kubwa ya iliyotolewa na Yesu pale alipojitoa kwa ajili yetu, alipe deni la dhambi zetu na kuifuta kabisa ili atupatanishe na Mungu.
Kwa hiyo, unapomkosea Mungu halafu ukamwendea kumuomba msamaha tena (kama vile Daudi, alivyofanya baada ya kuzini na kuua mtu),
Je, Ni tendo gani la majuto, ni dhabihu gani unajisikia moyoni mwako kwamba ni lazima umtolee Mungu?
Daudi alifahamu jibu la swali hilo wakati anamwomba Mungu amsamehe, aliomba pia Mungu arejeshe uhusiano mzuri kati yao.
Zaburi 51:17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
Usifikiri kwamba Mungu anatazamia kwamba utaongeza hela pale unapotoa sadaka kanisani –hapana. Hapendezwi na maua kama ishara ya toba. Wala hataki ubadilike kuwa mtawa. Yaani, anataka kitu kilicho kizito zaidi.
Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.