Dhana mpya Kabisa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mariko 9:35 Akaketi chini, akawaita wale Thenashara akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote.
Sababu kubwa ya watu kubishanabishana hapa duniani ni kwa sababu wanataka kujua ni nani aliye mkubwa; ni nani wa kwanza; ni nani anayeonekana kushangaza zaidi, ni nani kiongozi wa kundi. Na hii huanza tangu utoto
Kama una ndugu mliozaliwa pamoja, utakumbuka jinsi mlivyobishana-bishana. Mimi na dada yangu tulibishanabishana sana. Hii ni kawaida kwa watoto. Ndiyo maana ni nafasi ya mama na baba kuwafundisha watoto na kuwatiisha ili hatimaye wakue na kuachana na mabishano kama hayo.
Lakini kama tulivyoona jana, wanafunzi kumi na wawili wa Yesu, kumbe! Walikuwa hawajakomaa na kuachana na hali hiyo! Walikuwa wanashindania ni yupi aliye mkubwa katika kundi lao. Na wakati Yesu aliwahoji, waliaibika na kunyamaza tu kwa sababu walielewa kwamba bado hawajakomaa. Na kweli, lazima wangekuwa na aibu.
Tayari alikuwa ameshajua wanalolishindania. Ndiyo maana
Mariko 9:35 … keti chini, akawaita wale Thenashara akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote.
Hii ni kweli ambayo mtu mwenye uzoefu maishani ataelewa kabisa. Wanaotuhudumia zaidi, ndio tunaowaheshimu kuliko watu wote wengine.
Ni kwa sababu kwa asili, tuna ubinafsi na hatujakomaa. Unataka kweli kuwa wa kwanza, na mkubwa? Basi jua haya:
Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.