Endelea
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Nyakati 16:11,12 Mtakeni BWANA na nguvu zake; utafuteni uso wake siku zote. Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya; miujiza yake na hukumu za kinywa chake.
Wakati tumechoshwa, tunataka kuacha yote na kujiudhuru. Nguvu zinatupungukia, macho yanakuwa na gizagiza, mikono inalegea, na hata bidii yetu yakutimiza yale Mungu aliyetupa tuyafanye inatoweka pia. Kwa kweli, mtu akizidiwa, atapenda kujiudhuru na kuacha yote.
Nadhani sikosei nikisema kwamba sisi sote tunayo majira kama hayo maishani mwetu. Mwanzoni tulijaa matarajio mema na shauku moyoni kwa ajili ya maisha yetu … lakini sasa, hatuchangamki tena. Ni kipi kilichotokea?
Ni kama tumefikia njia panda – au tuendelee tu tukitumia nguvu ndogo tunazobakiza; au tuache yote na kurudi nyumbani. Tunafikia mahala pa kuamua hivi au hivi: Yote yananilenga mimi, lazima niendelee kuajibika, ni basi tu. Au la pili, kama Bruce Wilkinson alivyoandika katika kitabu chake, “Sala ya Jabez” … Nimeshafika mbali, lakini nimefikia pabaya. Kwa kuwa nimeshapoteza rasilimali zote ambazo ningepata, acha nikimbie haraka!
Lakini ungesemaje kama ningekwambia kwamba kuna chaguo lingine la tatu, chaguo bora kabisa.
1 Nyakati 16:11,12 Mtakeni BWANA na nguvu zake; utafuteni uso wake siku zote. Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya; miujiza yake na hukumu za kinywa chake.
Tunavyoweza kutimiza sisi kwa nguvu zetu ni vidogo sana ukivilinganisha na mambo ambayo Mungu anaweza kutimiza kupitia sisi, uwepo wake ukitushukia na nguvu zake zikituingia. Nisikilize, kamwe hukukusudiwa kutumika peke yako.
Mtakeni BWANA na nguvu zake; utafuteni uso wake siku zote.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.