Faida ya Kujiepusha na Uovu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 97:10-12 Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; huwalinda nafsi zao watauwa wake, na kuwaokoa na mkono wa wasio haki. Nuru imemzukia mwenye haki, na furaha wanyofu wa moyo. Enyi wenye haki, mmfurahieni BWANA, na kulishukuru jina lake takatifu.
Kuna njia mbili za kukabiliana na shughuli muhimu yoyote katika maisha. Kwanza ni kwa shingo upande, kama vile wengi wanavyofanya. Na njia ya pili ni ya washindi, kujitolea nafsi, yaani asilimia 100%.
Na kama vile maamuzi hayo mawili yanavyotofautiana sana; yakihusu kila kitu maishani – ndoa, kulea watoto, kazi, na lolote lile – lazima yatamhusu mtu anayeamua kumfuata Yesu.
Lakini kinachonihuzunisha ni kwamba, wengi wanapelekwa na uzembe. Yaani nia yao ni kuuliza, “Ninaweza kuchezea dhambi kiasi gani bila kukamatwa?” badala ya kuuliza, “Ninaweza kujikanaje na kutoa nini ili niweze kumheshimu Mungu kuliko vyote”
Bila shaka umeshakabiliana na maamuzi hayo. Ni kweli, Mungu anatuacha na uhuru wa kuchagua, lakini ni chaguo lipi anataka tulifanye.
Zaburi 97:10-12 Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; huwalinda nafsi zao watauwa wake, na kuwaokoa na mkono wa wasio haki. Nuru imemzukia mwenye haki, na furaha wanyofu wa moyo. Enyi wenye haki, mmfurahieni BWANA, na kulishukuru jina lake takatifu.
Mtu anapozembea bila kufikiria na kuwa na mahusiano na Yesu wa vuguvugu, lazima kule kuchezea dhambi kutampelekea kuasi kabisa akichochewa na waovu wanaotuzunguka.
Lakini tukifuata njia ya washindi, na kuangalia siku zote ni yapi tunaweza kuyafanya kwa kujitolea kwa ajili ya kumtukuza Mungu katika maisha yetu, tunajiepusha na uovu na kuuchukia … kumbe tunapata mafao mengi makubwa ambayo hatukutazamia:
Huwalinda nafsi zao watauwa wake, na kuwaokoa na mkono wa wasio haki. Nuru imemzukia mwenye haki, na furaha wanyofu wa moyo.
Chukia uovu!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.