Furahi na Ulie Pia
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 12:15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja na waliao.
Kuna utafiti uliyofanyika ambao unatisha sana. Kwa wastani, tutatumia karibia miaka 17 ya maisha yetu kwa kutazama skrini za simu zetu za mikononi. Ni masaha 145,800 au theluthi ya masaa yetu ya kuwa macho (yaani asilimia 33%). Jamani, hali hii inachanganya kabisa!
Tupitie tena mahesabu yale. Mfano, kwa siku moja una masaa 24, tuseme tunatumia masaha 8 kwa kulala usingizi. Inabaki masaha 16 kuwa macho. Tukitumia nusu kazini siku tano kwa wiki na theluthi kwenye simu inabaki nini? Masaha machache sana kufanya mambo mengine, machache tu.
Hali hii inaweza kuathiri kabisa mahusiano yetu na watu wengine. Ndoa zinaharibika. Watoto wanakosa ulezi. Matatizo makubwa ya kisaikoljia na ya kijamii yanaenea kama tauni ulimwenguni. Ni hali inayotisha kwa kweli.
Sasa tunaweza kufanyaje, wewe na mimi, ili tuvunje mzunguko huo? Tutumie busara iliyokuwepo daima kabla ya teknolojia ya kisasa, busara ya ki-Mungu na ya ki-Biblia kuleta tiba kwa ugonjwa huu uliopo katika jamii:
Warumi 12:15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja na waliao.
Ina maana, tafuta muda wa kutosha wa kutengeneza mazingira mazuri ya kihisia na ya kuchukuliana na watu wengine. Simama. Shangilia wakati mtoto wako anapata ushindi katika mchezo au akipiga hatua nzuri katika fani nyingine. Furahi kweli kweli na wafurahio.
Halafu wakati mtu anapata mateso, moyoni mwako, uumie pamoja naye. Uwe karibu naye, uketi pamoja naye na ikibidi ulie machozi pamoja naye.
Uwezo wa kuhisi maono ya wengine yakiwa ya furaha au ya maumivu una nguvu sana. Ni daraja inayounganisha watu wawili, tena ni daraja itakayodumu imara maisha yote. Ni daraja inayounganisha watu wawili na mara ingine, Yesu anaweza kuitumia kwa kuvuka upande wa pili.
Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja na waliao.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.