Habari Njema Angalau
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Timotheo 1:9 Ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele.
Siku hizi kupata habari njema ni kwa nadra sana. Mara unasikia kwamba mtu amechomwa kisu hapa, mwingine kupigwa risasi; kiwango cha riba kwa mikopo kimepanda, uchumi umeporomoka … nadhani umenipata. Labda ndiyo maana mashabiki wanapenda kusherehekea wakati timu yao inapata ushindi kwa sababu ndiyo habari njema pekee wanaopata.
Ni kweli, wachezaji wanapata ushindi wakijitahidi kufanya mazoezi magumu. Sisi washangiliaji tunapendezwa na mvutano huo wa kusubiri ni nani atakayeshinda. Yaani tunafuatana na timu yetu ikipanda au ikishuka … inakuwa burudani kwetu.
Lakini mtazamo huo ya kwamba lazima tuwe na mashindano daima, ni vizuri lakini ni kama tumeurithi. Tunataka sana kushinda, tunataka kufaulu kwa cho chote kile ambacho tumejaribisha. Sasa kwa mimi, mtu ambaye ana asili ya kupambana, kwa miaka mingi nilikuwa nimeanguka ndani ya mtego wa kufikiri kwamba maisha ni mashindano matupu. Kwa hiyo, iliniwia vigumu kukubaliana na dhana ya kwamba Mungu anaweza kunipokea hivi nilivyo.
2 Timotheo 1:9 Ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele.
Uhusiano wako na Mungu hauhusu swala la kushinda au kufaulu. Hauhusu kupata tuzo katika mashindano. Hauhusu kufaulu kufikia kiwango cha utukufu wake. Bali unahusu neema yake kwa sababu Yesu alishalipa gharama ya mapungufu yako yote, rafiki yangu … na mapungufu yangu pia.
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.