... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Habari Njema Mno

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 8:3,4 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili, ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.

Listen to the radio broadcast of

Habari Njema Mno

Download audio file

Je!  Wewe una ustadi gani katika kutii sheria na kanuni?  Kama una leseni ya kuendesha gari, ni lini uliwahi kuzunguka na gari bila kupita kiwango ya kasi inayoruhusiwa?  Hmm.

Kunshindwa kwangu kutii amri kumenishangaza tangu zamani.  Nililelewa katika nyumba yenye nidhamu ya Kijerumani.  Nilifuata mafunzo katika mazingira magumu ya kijeshi miaka minne ili niweze kuwa afisa katika jeshi letu.  Kama kungekuwa mtu angeweza kutii amri, angekuwa mtu kama mimi, sindiyo?

Lakini wala.  Kama vile wewe, nimeenda kinyume mara kwa mara.  Sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. (Warumi 3:23).  Kwa nini tunashindwa kutii amri jamani?  Labda tunataka kuzitii lakini hatuwezi.  Kuna sababu.  Isikilize:

Warumi 8:3,4  Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa  dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili, ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.

Mistari hiyo ilinichanganya kweli hadi pale nilipoweza kusoma maelezo mafupi ya mtu aliyeleta mabadiliko makubwa katika dini kwenye karne ya 16, mtu aitwaye Martin Luther.  Aliandika hivi:  “Sheria inagundua ugonjwa.  Injili ndiyo inayoleta tiba.”

Mungu alitenda yale ambayo sheria ilishindwa kufanya.  Alitoa uhai wake Yesu kwa kuharibu dhambi zetu.  Ni habari njema; habari njema mno.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.