Haki na Fadhili
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 21:21 Aandamaye haki na fadhili, ataona uhai na haki na heshima.
Hatua za kumfanya mtu kuwa mtu mzima zinahusiana na namna mtu anavyoweza kuleta uwiano kwenye mivutano mbalimbali ya maisha.
Kuna wakati wa kujenga na wakati wa kubomoa. Wakati wa kukumbatia mtu na wakati wa kuacha. Wakati wa kucheka na wakati wa kulia machozi.
Pia, kuna wakati wa kusimamia haki yako na wakati wa kulegeza msimamo wako ili uonyeshe upendo hata kama mambo hayajatengamaa, hata kama umekosewa kabisa.
Kwanini tunaongelea mambo hayo? Ni kwasababu siku hizi ukweli unapeperushwa, kila mtu anapiga kelele kudai kwamba anayosema yeye ndiyo kweli na watu wote ni lazima wakubali bila kuonyesha hata upendo mdogo.
Kusimamia ukweli ni muhimu kabisa, na inatubidi tuutafute. Lakini kila asubuhi nikiangalia taarifa za habari kwenye tovuti inayokusanya taarifa zinazoaminika, ninashangaa kuona namna watu wanavyopiga kelele bila kusikiliza watu wengine. Pia ninaona ambavyo wengi wetu hatuonyeshi tena adabu wala upendo kwa watu wengine.
Mithali 21:21 Aandamaye haki na fadhili, ataona uhai na haki na heshima.
Kuna watu wengi wanaojidai kuwa na haki siku hizi lakini kuna uhaba wa upendo. Wanaojidai haki ndiyo wengi, wanaoonyesha upendo nao ni wachache na hakuna uwiano kati ya pande hizi mbili.
Lakini Mungu anataka tufanye yote mawili – tusimamie haki lakini pia tuwe na fadhili. Sasa tukipata uwiano mzuri kati ya pande hizo mbili zinazovutana, Mungu ameahidi mafao yafuatayo: uzima, mafanikio na heshima.
Haki pamoja na fadhili. Huu ndio mpango wa Mungu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.