Hakuna Afananaye na Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 86:8-10 Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana, wala matendo mfano wa matendo yako. Mataifa yote uliowafanya watakuja; watakusujudia Wewe, Bwana, watalitukuza jina lako; kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, Wewe ndiwe mfanya miujiza, ndiwe Mungu peke yako.
Sasa niambie, je! Unalinganisha maisha yako kuwa kama safari ya msafiri anayetafuta kitu? Jibu la wengi wetu lingekuwa, hapana, sio sana. Unajua, tuko bizi sana. Shughuli ni nyingi. Pa kwenda ni pengi. Wa kuonana nao ni wengi.
Kwa upande mwingine, badala ya kuwa na shughuli nyingi, kuna watu wengine wanachoshwa kwa kukosa la kufanya. Kama vile wazee au maskini ambao hawana shughuli, hawana pa kwenda, hawana mtu kutembelea au mtu kuwatembelea. Kwa hiyo, wao, hawawezi kujiona kwamba wako safarini kwenda po pote, sidhani.
Sijui kama umegundua kwamba mwanadamu mara nyingi hua anatazamia kuona kitakachofuata? Likizo inayokuja, kuanza ajira mpya, hatua ingine maishani, kitu kile kimoja ambacho kitamletea amani, furaha, kuridhika, kustarehe – mambo ambayo daima yanaonekana kwamba mtu hawezi kuyafikia kweli.
Zaburi 86:8-10 Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana, wala matendo mfano wa matendo yako. Mataifa yote uliowafanya watakuja; watakusujudia Wewe, Bwana, watalitukuza jina lako; kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, Wewe ndiwe mfanya miujiza, ndiwe Mungu peke yako.
Kuna mchungaji akiwa pia mwanateolojia wa karne ya ishirini aitwaye Arthur Pink aliweza kueleza hivi: “Heri nafsi ya yule ambaye ameingiwa na hofu na mshangao kwa kuona ukuu na utukufu wa enzi ya Mungu.”
Rafiki yangu, hapa duniani hatutapata kamwe yale ambayo tunayatafuta. Hata kama miungu mingi midogo-midogo inayosimikwa pembeni ya njia katika safari yetu, yote ni bandia, ni mazingaombwe tu. Mungu tu peke yake ndiye awezaye kuridhisha hamu ya moyo wako, kwa sababu ndiye Mungu peke yake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.