... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hali Inayoleta Ongezeko

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Matendo 9;31 Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.

Listen to the radio broadcast of

Hali Inayoleta Ongezeko


Download audio file

Mtu akifuata vyombo vya habari, ataambiwa kwamba kanisa hua linafifia.  Habari hii inawafurahisha makundi mbali mbali ya wapinzani.  Lakini hao waandishi wa habari hawatangazi jinsi kanisa linaongezeka sana sehemu nyingi duniani, kwamba linajengwa na kustawi vizuri.

Vipi?  Wewe unaonaje?  Unafurahi kusikia kwamba watu wanazidi kubadilika kuwa Wakristo, au labda habari hiyo inakutisha kwamba inaturudisha kwenye siku za kale ambazo zilipitwa na wakati?  Hailishi uko upande gani, ujue tu kwamba vituo vya mayatima, mahospitali, shule nyingi, vyuo na misaada kwa maskini na waliotengwa – haya yote katika historia, yametokana na jitihada za Wakristo duniani kote.

Sasa ni yapi yanasababisha kanisa moja kustawi na kukua wakati kanisa lingine linadumaa?  Sikiliza tena mstari tuliosoma jana:

Matendo 9;31  Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.

Katika lugha ya siku hizi, wengine wangesema kwamba kanisa wakati ule lilikuwa na uamsho.  Ni vipi vilivyosababisha wakue na kuongezeka?  Kwanza, waliishi kwa amani, pili, walimheshimu Mungu na kumtii.  Kwa hiyo walipata baraka na waliwezeshwa na Roho yake Mtakatifu.

Kumbe!  Inaonekana kwamba uamsho hua unatokea wakati Wakristo wanaanza kutii Neno la Mungu!

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy