Hatari za Dini
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 5:16-18 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato. Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi. Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.
Ni ajabu sana jinsi ilivyo rahisi mtu kuvichukua rehema zake Mungu na neema yake – hata kama vinashangaza – na kuvibadili viwe orodha ya kanuni na makatazo tu. Mtu akifanya hivyo atakuwa ametengeneza nini? Atakuwa ametengeneza dini.
Kwa njia fulani, inaeleweka kwa sababu Habari Njema ya Yesu kwa kweli inalenga rehema zake Mungu pamoja na neema yake, lakini pia inatudai mwitikio – kuvipokea kwa imani katika toba. Sasa, kadiri mtu anavyokusudia kuachana na dhambi zake, ndipo inazidi kuwa rahisi kwake kuangukia kwenye mtego wa kujitengenezea kanuni nyingi za kumsaidia njiani.
Lakini kadiri mtu anavyojitahidi kuzifuata, ndipo atazidi kufeli. Halafu kadiri anavyofeli, ndipo atazidi kupelekwa kwenye njia ya amri zilizoorodheshwa kama dini. Hatima yenye mantiki ya mfumo huo itakuwa kama ilivyotokea katika mistari ifuatayo:
Yohana 5:16-18 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato. Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi. Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.
Yesu alikuwa amemponya kiwete siku ya sabato lakini viongozi wa dini hawakufanya kingine tofauti na kumshambulia. Si kwamba alivunja sheria tu lakini alijilinganisha na Mungu pia.
Hayo yaliwachukiza mno watu hawa wa dini kiasi cha kuwasukuma kutafuta njama ya kumwangamiza. Ni kweli?! Ametoka kumponya jamaa huyu!
Kama vile mwanamuziki maarufu duniani aitwaye Bono alivyosema, Roho Mtakatifu akiondoka ndani ya jengo, kinachobaki ni dini tu! Usitugeukie kuwa mshikilia dini, tafadhali!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.