... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hatua Tatu za Maisha

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 6:10-21 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusiko haribika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwakuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyowako.

Listen to the radio broadcast of

Hatua Tatu za Maisha


Download audio file

Kejeli inayohusu mali ni kwamba inaweza kuanza kumtawala mtu kwa urahisi kabisa.  Yaani baraka zile ambazo Mungu ametukirimia kwazo kwa ajili ya manufaa yetu tuweze kuzifurahia, mara nyingi zinageuka kuwa kama mabwana wa kututawala.

Inasemekana kwamba kuna hatua kubwa tatu maishani.  Kutamani kupata vitu,  kukusanya vitu, na kupunguza vitu.  Katika ujana wake, kwa kawaida, mtu hana uwezo wa kipesa wa kununua vitu anavyotamani sana, kwahiyo anaendelea kutamani kuvipata tu.  Mimi ninakumbuka wakati nilikuwa kijana, nilitamani sana kupata siku moja, rediondogo. 

Halafu, wakati mtu anakuwa mtu mzima, anaanza kukusanya vile vitu alivyokuwa anavitamani zamani na hata vingine zaidi.  Hiki nakile.  Wengine wanakusanya vingi sana hadi inabidi wakodi kontena pa kuvihifadhi kwa sababu havienei ndani ya nyumba!

Hatimaye, katika miezi ya mwisho ya maisha ya mtu, kama vile ilinibidi nifanye kwa ajili ya mama yangu mzee, lazima vitu mtu alivyotunza vig awanywe au vitupwe.  Mama yangu hakuwa na vituvingi, lakini hata hivi ilitubidi tukodi gari lenye kokoteni kupeleka karibu vyote kwenye dampo.  Je!  Unaonaje?  Inaeleweka kweli?  Yesu alisema hivi: 

Mathayo 6:10-21Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, nawevi huvunja na kuiba; bali jiwekee ni hazina mbinguni, kusiko haribika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwakuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

Ni kweli, nijambo jema kutunza vitu.  Vingine vinaweza kuwa baraka kabisa.  Lakini mali ikianza kukuta wala, inageuka kuwa laana kubwa mno. 

Msijiwekee hazina duniani.

Hilindilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwaajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy