... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hekima Iliyokuwepo Kabla Dunia Haijaumbwa.

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 2:6,7 Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanoitawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa ambayo Mungu aliiazimu tangu milele kwa utukufu wetu.

Listen to the radio broadcast of

Hekima Iliyokuwepo Kabla Dunia Haijaumbwa.


Download audio file

Sehemu za gazeti au kwenye mtandao zinazosimulia jinsi mtu anavyoweza kujiinua mwenyewe, zimejaa hekima ya kidunia inayoshawishi kwa njia mbali mbali, zingine za ajabu-ajabu na zingine zinazoweza kuathiri mtu hata kuhatarisha uhai wake.

Kama ni imani ya kumfikia Mungu kwa fikra, au kama ni ushauri unaopingana kuhusu mlo uliyo bora, au kama ni jinsi mwanamke fulani aliyefanya kibarua kama kahaba na kuharibu ajira yake (hii ni mifano mitatu niliyoweza kusoma leo hii tu) ni rahisi mtu kufikia maamuzi kwamba dunia hii imeshapasuka.

Lakini hata hivi, ushauri huu potovu unapokelewa kuwa hekima na jamii isiyoshuku.  Tangu miaka mingi, magazeti yanayolenga akina mama yameeneza takataka kama hiyo.  Najiuliza kama wewe umewahi kudanganywa na mambo kama hayo.

Sasa, kinyume cha hayo, tumsikilize Mtume Paulo akiandikia kanisa lenye matatizo ambalo lililoweza kupotoshwa na udanganyifu huo miaka elfu mbili iliyopita:

1 Wakorintho 2:6,7  Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanoitawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa ambayo Mungu aliiazimu tangu milele kwa utukufu wetu.

Sawa, najua kwamba hekima ya Mungu labda haina mvuto kama vile mambo ambayo ulimwengu huu unaoweka mbele ya macho yetu, lakini pendo, heshima, unyenyekevu, msamaha, wema … tunajua kwamba hapo ndipo hekima ya kweli ipo.  Pia tunafahamu kwamba hekima hiyo  ya Mungu inafanya kazi kweli kweli.

Usidanganywe na hekima bandia ya watu wanaobatilika.  Kwa sababu Mungu aliazimu kutupa hekima yake tangu milele kwa utukufu wetu.

Na, Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy