Hekima ya Kale (1)
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Tito 2:1,2 Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima; ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi.
Hivi umewahi kuchukua kitabu cha zamani na kukisoma, halafu ukaona kama kimepitwa na wakati!? Mitazamo ile na namna uliwengu ulivyokuwa zamani … haina uhusiano na sisi wa leo.
Mara kwa mara, mtu fulani atapost tangazo la zamani kwenye mtandao wake wa kijamii kutoka gazeti kwenye la zamani, kwamfano, nafasi ya wanawake zamani kwenye miaka ya 1950. Nafasi yao ilikuwa nyumbani ilikuwa ni kufagia, kufanya usafi na kupika chakula.
Pia, Biblia inaonyesha nafasi ya kila jinsia na mtazamo wa watu katika karne hii ya 21.
Kwahiyo, kuanzia leo na kuendelea, tutachunguza kitu kinachoitwa, “hekima ya awali”, kuhusu nafasi ya wanaume na ya wanawake katika ulimwengu wa leo nikianzia na mistari ifuatayo:
Tito 2:1,2 Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima; ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi.
Kama Biblia isingelenga maisha ya kila siku, basi isingetufaa. Anachokisema Paulo hapa akimwambia mwanafunzi wake Timotheo, ni kwamba lazima awafundishe watu wote kuishi kulingana na Neno la Mungu.
Anaanza na watu muhimu kabisa ambao ni wanaume wazee. Kwanini? Kwa sababu nafasi yao ni kuwa vielelezo. Wanapaswa kuwa mifano mizuri ya kufuatwa.
Ninyi wazee, watu wanawatazama sana, kwahiyo sikilizeni ushauri huu wa kale. Kila mmoja wenu awe na kiasi, awe mstahivu, mwenye busara, awe mtu mzima katika imani na upendo na saburi. Yaani watu wanakuchunguza sana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.