... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hekima ya Kale (3)

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Tito 2:5 Na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.

Listen to the radio broadcast of

Hekima ya Kale (3)


Download audio file

Sawa, sasa leo … leo kabisa; tunataka kupambana moja kwa moja na siasa ya usahihi wa kisasa. Tena tutatumia Neno la Mungu lenyewe.  Hapo ndipo kuna mvutano mkubwa kati ya mtazamo wa kibiblia na mtazamo wa ulimwengu wa leo usiomcha Mungu.

Kwahiyo, nafasi ya mwanamke katika ulimwengu wa leo ni ipi?  Inategemeana na nchi unayoishi.  tamaduni mbalimbali zina mitazamo tofauti-tofauti kuhusu mada hii.  Lakini zaidi na zaidi, wanawake wanajaribu kufanya kazi mbili – wanaajiriwa na wanatunza mambo ya nyumbani pia. 

Jana tulijadili swala la wanawake wazee – kuwa kielelezo cha kuigwa kwa ajili ya wanawake vijana katika jamii, kuwafundisha yaliyo mema.  Lakini sasa tumefikia maneno yasiyoendana na siasa ya leo, yaani yanaenda kinyume kabisa ya mtazamo ule: 

Tito 2:5  Na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe. 

Zamani, kwenye karne ya kwanza baada ya Kristo, nafasi ya mwanamke ilikuwa ndani ya nyumba; kupika chakula, kufanya usafi, kuzaa watoto na kuwalea.  Mazingira yamebadilika sana tangu siku hizi.  Kwahiyo … tufanyeje sasa!, au tuutumiaje msatari huu katika karne  hii ya 21, mmh … ? 

Hata kama mazingira yamebadilika sana, wanawake bado wana nafasi kubwa katika maisha ya familia.  Mimi, kama mume, ninapenda kumhudumia mke wangu.  Na yeye, kama mke, akiwa mke wangu, anapenda kunihudumia pia. Tunatofautiana kila mmoja katika kumhudumia mwenzake, lakini bado tunahudumiana, tunajaliana kama vile ilivyokusudiwa. 

Kwahiyo, akina mama, muwe na busara, muwe safi, tunzeni vizuri nyumba zenu, muwe wafadhili mkiwa tayari kuwahudumia waume zenu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly