... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hisia au Maadili

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 11:3 Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.

Listen to the radio broadcast of

Hisia au Maadili


Download audio file

Hisia za mwanadamu ni sehemu kubwa sana ya nafsi yake.  Mtu hawezi kupuuza hisia, tena haimpasi kuzipuuza.  Lakini pia, hisia zinazo uwezo mkubwa wa kutupotosha.

Kila Taifa katika ulimwengu huu litakuwa katika tabaka mojawapo kati ya hizi mbili: mataifa ambayo sheria zake zinasimama juu ya maadili ya Kiyahudi na Kikristo na mataifa yasiyo na maadili yale.  Sasa katika tabaka ya kwanza kuna sehemu mbili: mataifa yaliyoambatana na maadili yale (yamebaki machache). 

Kadiri mtu anapelekwa mbali na njia za Mungu – Mungu mmoja wa kweli, Mungu aliyetupenda kipekee hadi akamtuma Yesu kufa msalabani ili atuokoe – kadiri tuanoenda mbali naye, ndipo tutazidi kuhama kutoka kwenye maadili mazuri na kufuata hisia zetu tu. 

Kama nimeshasema, hisia zenyewe ni muhimu, tena hatupaswi kuzipuuza.  Lakini wakati hisia zinanaanza kutawala maadili na kuyafuta, kumbe tunaingia eneo la hatari kabisa.

Mithali 11:3  Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. 

Uaminifu, utu wema, kuheshimiana, fadhili, kuthamini uhai wa binadamu … maadili hayo yanayo mizizi mirefu sana kuliko hisia tu.  hata kama hisia zetu ziko kinyume kabisa, zikijaribu kutuongoza kwenye njia mbaya. 

Angalia, hisia zinapanda na zinashuka.  Kuna mara zinatusaidia kweli, lakini mara nyingi zinatusaliti wakati ukaidi wa moyo wa mwanadamu unapotutawala, si kweli? 

Usiache maadili yaliyowekwa na Mungu kwa sababu hujisikii tu.  Acha uadilifu wa wenye haki ukuongoze. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.