Hofu, Amani na Faraja
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Matendo 9:31 Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
Kwa kweli tunaishi katika kipindi cha hatari. Ukinunua gazeti utasoma jinsi wenye mamlaka, si kila mara lakini mara nyingi wanatenda visivyo. Pia, makanisa mengi yamejaa ufisadi na matumizi mabaya ya fedha. Ni kipi kinachoendelea?
Sijui kama wewe unaenda kanisani au la, lakini tafadhali, chukuliana nami. Kanisa, Wakristo … si wakamilifu. Kwa kweli, hawajawahi kuwa wakamilifu … tangu karne ile ya kwanza wakati ilimbidi Mtume Paulo kuandika barua za makaripio kwa makanisa kaidi yaliyokosa nidhamu.
Ni huzuni kubwa kwa sababu kati ya tasisi zote, kati ya kundi la watu duniani, kanisa halipaswi kuwa hivi, si kweli?
Sasa mtu angefanyaje? Angekabilianaje na hali kama hiyo ili alete matengenezo yanayotakiwa? Kanisa la kale liliteswa sana na mateso yanalijia tena siku hizi. Lakini sikiliza kwanza yafuatayo:
Matendo 9:31 Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
Kumcha Mungu si kumwogopa, bali ni kumstahi na kumheshimu na kumtii. Ni kweli, kwa mtu aliye nje ya Ukristo, kuna mambo mengine Wakristo wanaamini ambayo hayaeleweki. Lakini hata ukiwa wapi kuna jambo moja lisilopingika: Kuna wakati watu wa Mungu wanamheshimu kweli kweli badala ya kuchezea dini, mambo mazuri hua yanatokea, mazuri sana.
Hata kama hayo mazuri hayatangazwi kwenye vyombo vya habari, kuna mambo mema mengi yanatokea. Ni matokeo ya jinsi watu wa Mungu wanaenenda katika kicho cha Bwana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.