Imani iokoayo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waefeso 2:8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu.
Imani ni jambo jema kabisa kuwa nalo, hususani pale imani yetu iko ndani ya kitu au mtu ambaye hawezi kutuangusha. Lakini je! Imani yako ikoje kipindi kigumu cha maisha? Je! Imani yako ni imara kama mwamba au kuna mara inayumba-yumba?
Wakati njia yetu ina visiki na vikwazo, imani yetu inatikiswa sana na tunaweza kuwa na mashaka kwamba labda Mungu hatupendi tena, labda dhambi zetu na mazingira tuliomo vimehatarisha hali yetu ya kukaa naye milele.
Adui wako Ibilisi anataka kukutenganisha na neema thabiti ya Mungu ambayo ingekulinda salama leo, kesho, na hata milele. Halafu kadiri anafaulu kututenganisha nayo, ndipo tunazidi kwenda mbali na Mungu – ndivyo inavyosikika kwetu.
Najua ya kwamba kuna mtu leo, sehemu fulani duniani, ambaye anafuata kipindi hiki, mtu ambaye amekatishwa tamaa hivyo. Na kama leo haupo sehemu kama hiyo, siku moja unaweza kujikuta mashakani.
Waefeso 2:8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu.
Imani yangu na imani yako kamwe isijengwe juu ya uwezo wetu wa kutenda mema au kumheshimu Mungu kwa sababu uwezo huo si imara.Uwezo wa Mungu ni wa uhakika, kwa sababu kujitolea kwake hakuwezi kutuangusha hata siku moja.
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.