Imani Yako Isiwe na Unafiki
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Timotheo 1:5 Nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.
Kuamini kitu kilicho nje yetu ni sehemu ya asili ya binadamu. Kila mmoja wetu atafikia hatua ya kutafuta “kitu” hicho cha kuamini; “kitu” kinachostahili kuaminiwa.
Wakati bado tunakitafuta “kitu” hicho kimoja, kuna maswali mawili lazima tujiulize. La Kwanza ni hili: je! Nimekipata kilicho sahihi? Pili, je! Ninakiamini kweli kweli?
Kuna wengine wanaweka imani yao katika uchumi na kadiri mtu anatajirika, ndipo inamwia rahisi kuendelea kutegemea mali. Wengine wanaweka imani yao katika vipaji vyao na uwezo walio nao. Wengine wanaweka imani yao katika heshima ya ulimwengu huu kadiri wanavyofanikisha juhudi zao walizozichagua. Halafu kuna wale ambao, baada ya kugundua kwa kupitia misiba mbali mbali kwamba yale yote yanawaangusha tu, hatimaye wanaweka imani yao kwake Yesu.
Hawa sasa, swali lile la kwanza ni rahisi kwao kulijibu. Ndani ya Kristo, tuna uhakika kwamba tumepata kitu kilicho sahihi kabisa. Lakini je! Swali la pili, tunaweza kulijibuje? Je! Ninamwamini kweli kweli? Umsikilize Paulo akimwandikia mwanafunzi wake Timotheo:
2 Timotheo 1:5 Nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.
Imani isiyo na unafiki. Hmm. Je! Imani kama hiyo inafananaje? Ni imani isiyojiendesha pembeni majira mazuri; pia ni imani inashikilia sana Mwokozi wake wakati wa dhoruba na tufani.
Ni imani inaendelea kumtazama Yesu licha ya hali ya mazingira ikijua kwamba kamwe hawezi kutuangusha.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.