Imekuja Ghafla!
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 1:14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Tayari! Tumefika! Ghafla, tunakuta ni sikukuu ya Krismasi. Kwa hiyo acha nianze kwa kukutakia na wapendwa wako wote kheri zote za Krismasi – kwa sababu hailishi hali yako ikoje, wala mazingira yako yakoje, leo ni siku ya kipekee kabisa … kwa ajili yako.
Sawa, najua labda umeshasherehekea Krimasi nyingi sana kabla ya leo. Pengine sikukuu hii imekuwa kwako kama kawaida. Lakini Krismasi, hata kama inakuja kila mara kwa kalenda ya mwaka kwa tarehe ile ile, si ya kawaida, hata kidogo.
Acha nikuulize, Je! Kama Mungu angetafuta kukwambia neno. Kama angetaka ujue jinsi anavyokupenda, angetumia njia gani? Ingeonekanaje? Jibu ni kwamba ingefanana na tukio tunalolisherehekea kila Krismasi.
Yohana 1:14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Kwa nini Yohana anamtambulisha Yesu kuwa “Neno”? Ni kwa sababu Yesu, Mwana wa Mungu, ndiye Mungu anayeongea nasi kwa lugha inayoeleweka. Yesu ni Mungu anayetukaribia kwa mahusiano ya undani – kwako na kwangu pia – akisema, “Ndivyo nilivyo. Hii inaonyesha ninavyokupenda kwa kuwa nimemtuma Mwanangu pekee ili uweze kunijua. Ili kwa kuamini alichokifanya kupitia kifo chake pale Msalabani, uweze kusamehewa. Ili, kupitia ufufuo wake, uweze kupata maisha mapya, uzima tele na wa milele.”
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.