Inua Macho Yako Juu Mbinguni
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 40:26 Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumbe hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hofdari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.
Tumefika. Leo ni siku ya kwanza ya mwaka mpya. Kwa hiyo nakutakia kheri za mwaka huu licha ya changamoto yo yote ile itakayokukabili. Na tukisema ukweli, hatujui lo lote kuhusu yatakayotokea mwaka huu.
Tarehe hii hii, miaka 100 iliyopita, kulikuwa mtu aliyeitwa Edwin Hubble alitoa hotuba ya sayansi kwenye kongamano lisilofahamika sana. Sasa siku ile ya kawaida, kwa tarehe ile ya kuanza mwaka mwingine mpya, kulitokea jambo la ajabu kabisa. Gazeti Ugunduzi inaitambua siku ile, kuwa “tarehe ya kipekee katika historia ya sayansi.”
Kupitia utafiti wake aliufanya taratibu-taratibu na uchunguzi wake, Hubble alibayanisha habari ya uwepo wa makundi mengine ya nyota na sayari tofauti; kwamba mawingu yenye rangi yanayoonekana mbinguni si mawingu ya gesi, kama vile Nebula ya Andromeda, bali ni makundi mengine ya nyota, yaani magalksi mengi yaliyotawanywa kote mbinguni. Siku ile, ndipo ugunduzi wa viumbe vinavyojaa mbingu ulipoanzia.
Sasa wewe na mimi, leo tunaweza kutazama nyota miliyoni zinazoonekana kwenye galaksi yetu iitwayo Njia ya Maziwa, tukifahamu kwamba ni idadi ndogo sana ya nyota matriliyoni zinazopatikana mbinguni – na hatujui zinaishia wapi.
Isaya 40:26 Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumbe hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hofdari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.
Wakati mwingine tunaanza mwaka mpya kwa kuyumba-yumba. Bila shaka tutakutana na vikwazo njiani. Lakini ukweli ni kwamba Mungu aliyeumba jeshi hizi zote za mbinguni, akijua jina la kila nyota, ni Mungu yule yule anayekupenda kipeo kwa kiwango kisichoelezeka. Mungu anao uwezo na nia kukuongoza na kukupitisha katika yote ambayo utakabiliana nayo mwaka huu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.