Jaribu la Kwanza
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 4:1-4 Mathayo 4:1-4 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Adui yako, Ibilisi, ana tabia nyingi mbaya sana. Tabia moja mbaya mno aliyonayo nikukukandamiza wakati umeshaanguka. Anasubiri pale ambapo hauna nguvu, halafu anakushawishi akikuletea tiba ya bandia.
Hakuna anayetaka mateso, hata hivyo hatuna budi kupitia mateso mara kwa mara. Kuna mateso makubwa kuliko yote niliyoyapitia karibia miaka 30 iliyopita wakati nimesalitiwa. Kusema ukweli, kidogo nife.
Lakini sasa nimegundua kwamba ilikuwa fursa nzuri kuliko zote Mungu alizonipatia. Ndio maana jaribu la Yesu katikati ya mateso yake, linaeleweka vizuri kwangu mimi leo hii.
Mathayo 4:1-4 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Unapoteswa na jaribu analokuletea Shetani, usijaribu kumaliza mateso kwa nguvu zako binafsi. Yesu angeliweza kubadilisha mawe yawe mikate lakini hakufanya hivyo, aliamua kumtegemea Mungu na kusimama imara katika Neno lake.
Mateso huwa hayaeleweki pindi mtu anateswa, lakini katikati yake, inawezekana akapata fursa kubwa katika maisha yetu. Kwa hiyo usitapanye bure kwa kuangushwa na jaribu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.