... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Jaribu la Pili

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 4:5-7 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; na mikononi mwao watakuchukua; usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

Listen to the radio broadcast of

Jaribu la Pili


Download audio file

Sijui kama umwewahi kumjaribu Mungu?  Yaani unakuta mtu anapitia kipindi kigumu sana halafu anakuja mbele za Mungu na kudai, “Bwana, kama kweli unanipenda, muda umewadia wa kunionekania.”

Haujambo! Mimi ni Berni Dymet na ninakukaribisha kwenye kipindi hiki cha NENO SAFI NA LENYE AFYA.

Kwa mtazamo wetu sisi binadamu, wazo letu ni la mantiki.  Mungu ananipenda, mimi ninaumia, kwa hiyo lazima aje kuweka mambo sawa ili nisiendelee kuteswa. Kweli Bwana, mimi nitafanya usiponionekania, nitaharibikiwa.  Si inaeleweka kwani!?

Wakati Yesu alipokuwa anateseka jangwani, kumbe Ibilisi alimjia na kumjaribu; yaani amjaribu Mungu. mtu anaweza kusema kwamba ni hatari, si kweli?

Mathayo 4:5-7  Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; na mikononi mwao watakuchukua; usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.  Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

Kwahiyo, tujiulize.  Kwa nini tusimjaribu Mungu?  Kwasababu bila shaka ana lengo lililofichwa katikati ya mateso yetu, kufanya kazi ndani yetu au kuwasaidia watu wengine … lengo lisiloweza kujulikana muda huo huo.  Tukidai abadilishe mwelekeo wake, ni kama kukashfu mamlaka yake, na kumwambia aachane na kusudi lake maalum ili sisi tupate kustarehe kwenye anasa!

Usimjaribu Bwana Mungu wako.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

 


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy