... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Je! Bado Unajaribu Kuvutia Watu Wengine?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 3:23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu.

Listen to the radio broadcast of

Je! Bado Unajaribu Kuvutia Watu Wengine?


Download audio file

Haijalishi tunavyofikiria kwamba tu wanyenyekevu kiasi gani, bado kuna kishawishi kilichofichwa kwenye kiini cha mioyo yetu kinachotwambia kwamba ingependeza sana kama sisi tungeweza kuvutia watu wengine.

Daima inanichekesha kwamba wakati tunajiona kuwa wanyenyekevu – mimi ni mnyenyekevu! – kumbe!  Tayari tumeisha kuwa na kiburi.  Lakini kwa kweli, kuzidi kuwa na unyenyekevu ni kuwekwa huru, jambo jema ambalo linatuweka huru na shinikizo kubwa wa kufikiri kwamba lazima tuvutie watu wengine.

Tukisema ukweli, watu wengine ni kundi lenye kigeugeu.  Wale wale walioshangilia mahubiri ya Yesu yenye nguvu na miujiza yake ya kushangaza, ndio waliopiga kelele wakisema “Umsulibishe!” wakati alisimama mbele ya Pontio Pilato sikukuu ile ya Pasaka.

Naomba uwe mkweli ukijikagua kidogo.  Jinsi unavyoishi, ninyi akina mama – jinsi unavyohangaikia mitindo ya nywele zako na jinsi unavyojipaka vipodozi; na ninyi wanaume, jinsi unavyochagua tai utakayovaa ofisini ili uonekana kuwa bosi – au cho chote kile ambacho unavyoweza kufanya kwa kujiandaa katika mazingira yako … Je!  Ni kwa kiasi gani maamuzi yako unafanya kwa lengo la kuvutia watu wengine?

Kwa sababu kufanya hivyo kunaweza kukupelekea katika vifungo vya utumwa, hali ambayo Mungu alikuwa anataka kukuweka huru kwavyo.

Wakolosai 3:23  Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu.

Kwa vyo vyote, katika yote unayofanya, jaribu kutenda vizuri iwezekanavyo.  Lakini badala ya kutumia vipaji vyako ulivyopewa na Mungu ili uwavutie wengine, vitumie kumtukuza Mungu.  Hapo ndipo kuna uhuru.  Hapo ndipo mtu anaweza kupata kuridhika kweli kweli.

Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy