Je! Biblia ni Hadithi za Kusadikika za kitoto!?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 55:10,11 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Je! Biblia ni Hadithi za Kusadikika za kitoto!?
Download audio file
Tukiwa wa kweli, kitabu ambacho Wakristo wanakiita “Biblia” kina matukio ya ajabu mnoo ambayo ni vigumu mtu kuyaamini. Yesu kabadilisha maji kuwa divai; Yesu katembea juu ya maji. Mmm!, jamani, hivi ni kweli?, Au ni hadithi za kusadikika tu!.
Kutokana na utafiti uliofanywa na taasisi ya kusaidia Wakristo wanaoteswa, taasisi iitwayo Sauti ya Wafia Dina, uliofanyika katika nchi 52 duniani, Utafikit huo unasema hivi, ni vigumu mno mtu kupata Biblia, na sehemu zingine ni Atari kabisa mtu kuwa nayo. Zimepigwa marufuku, na hata kuziuza inaonekana kama ni biashara haramu.
Sasa kama Biblia ni hadithi za kusadikika tu, sasa ni kwanini imepigwa marufuku kwenye nchi 52?…Mtu mmoja alisema hivi, Haiwezekani mtu kufungwa gerezani kwa kusoma tu hadithi za watoto, sasa kama ni hivyo, ni kwanini wanaipiga marufuku?…Haieleweki.
Biblia imepigwa marufuku kwasababu ni ujumbe wa kweli wenye nguvu unaoweka watu huru na kuwabadilisha kuliko habari nyingine yoyote hapa duniani. Biblia imepigwa marufuku kwasababu ni Mungu anaongea na watu wa kawaida kama wewe na mimi kupitia Neno lake, anaachilia uweza wake kutimiza makusudi yake.
Isaya 55:10,11 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Ndio maana wanaipiga marufuku. Biblia si hadithi za watoto, Ni uwezo wa kubadilisha maisha yako kabisa. Ni uweza wa Mungu unaofanya kazi ndani yako na kupitia wewe ili atimize makusudi yake kwa ajili ya utukufu wake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.