Je!, Mtu Anaweza Kujua Kweli Kweli?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 1:8,9 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
Wakati unakosea – namaanisha unapokosea san asana, – unaweza kuamini kwamba Mungu atakusamehe kweli?. ni jambo gumu kupokea msamaha huo; yaani kujisamehe mwenyewe.
Juzi nilikuwa naongea na mwanamke mmoja aliyewahi kufanya makosa makubwa maishani mwake. Sasa, anamuamini Yesu kwa moyo wake wote; pia anamtumikia kwa bidii zote akijitolea mwenyewe kwa vipaji na vipawa alivyo navyo. Lakini ilikuwa dhahiri kwamba alishindwa kuachana na makosa yale aliyoyafanya miaka mingi iliyopita.
Kwahiyo, nilimpa changamoto ifuatayo, “Najua kwamba unafahamu, lakini je! Unajua kwelikweli?” Na ilikuwa dhairi kwenye kiini cha moyo wake kwamba jibu ni … hapana. Ndio, alifahamu akilini, alijua kwamba kwa kumwamini Yesu, alipata msamaha. Lakini alikuwa hajaupokea msamaha huo moyoni mwake; minyororo iliyokuwa imemfunga ilikuwa haijavunjwa bado.
Yamkini unajikuta kwenye sehemu kama hiyo, kama bado umeshindwa kujisamehe ili uwe huru, Kusema ukweli, lolote ninaloweza kulisema halitaweza kuvunja pingu hizo. Lakini habari njema ni kwamba, Mungu anatamka uwezo wake unaofanya kazi na minyororo huwa inakatwa. Kwa hiyo … tumsikilize Yeye akiongea kwa nguvu:
1 Yohana 1:8,9 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.