Je! Mungu Ananisikiliza Kweli?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 1:5-6 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
Je! Umewahi kutembelewa na mtu aliyekuomba ushauri na ulipomshauri, ulijiuliza kwa nini alikujia? Ni kama hataki kujua. Ni kama hakusikilizi.
Mwanangu mmoja, akiwa ana miaka arobaini na kidogo sasa, alinjia hivi karibuni akiomba ushauri kuhusu swala gumu alilokabiliana nalo. Kwanza kabisa, kama mzazi wake, niliona ni fursa kubwa kwangu yeye kuniomba ushauri. Pili, ni dhairi kwamba nilijaribu kumwonyesha jinsi anaweza kutumia hekima. Ilikuwa furaha kwangu kabisa.
Mimi nahisi kabisa kwamba ndivyo ilivyo kwa Mungu pia, wakati tunamwomba atupe hekima yake.
Yakobo 1:5-6 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
Jana tuliweza kuchunguza sehemu ya kwanza ya mstari huu. Lakini sasa tutafakari sehemu ya pili. Je! Unafikiri mwanangu, wakati alinijia, kwamba angekuwa na shaka (hata kwa sekunde moja) kwamba labda nisingempa ushauri bora? Hapana, isingewezekana!
Kwa nini sasa tunamtilia Mungu mashaka wakati tunamwendea tukiwa na shida kubwa na kuomba, “Bwana nisaidie kwa hili. Kwa nini nisione mwanga? Nawezaji kulipitia?” Tunajiuliza kama kweli yupo, sembuse kama anatusikiliza.
Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.