Je! Mungu Bado Anatuadhibu?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Ufunuo 3:19,20 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
Acha nikuulize, je! Mungu bado anaadhibu watoto wake? Wakati unafanya kosa na unajua ni kosa, je! Bado anachukua fimbo yake kubwa na kukuchapa mkono?
Ni swali zuri la kuuliza na zuri la kulijibiwa pia kwa sababu katika ulimwengu huu unaoendeshwa na usababisho na matokeo, matazamio yetu ni kwamba waliotenda uovu lazima waadhibiwe.
Lakini bado kuna swali hapo. Mtu akiamini kwamba Yesu alikufa pale msalabani ili alipe gharama ya dhambi zake, anafahamu kwamba alichukua adhabu yake juu yake mara moja na kwa mara zote. Kwa hiyo isingeeleweka Mungu kumwadhibu tena, au je? Hata Yesu mwenyewe alisema hivi:
Ufunuo 3:19,20 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
Sasa je! Mungu bado anatuadhibu? Jibu ni hapana. Je! Anatukemea na kuturudi kutokana na upendo wake mkubwa kwetu? Ni kweli kabisa. Kwa nini? Anataka kutufundisha, kuturejesha kwake, na kushirikiana nasi.
Kuna utofauti mkubwa kati ya nidhamu na adhabu. Kuna mwandishi aliyepata tuzo aitwaye L.R. Knost aliweza kueleza hivi: “Nidhamu ni kumsaidia mtoto kutatua tatizo. Adhabu ni kusababisha mtoto ateswe kwa sababu ya tatizo lake.” Yesu analenga utatuzi, halengi tatizo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.