... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Je! Mungu Unanisikiliza?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 86:6,7 Ee BWANA, uyasikie maombi yangu; uisikilize sauti ya dua zangu. Siku ya mateso yangu nitakuita, kwa maana utaniitikia.

Listen to the radio broadcast of

Je! Mungu Unanisikiliza?


Download audio file

huu ni Ulimwengu ambao kuna kelele nyingi za sauti zinazoshindana, maoni tofauti, jumbe mbali mbali kwenye mtandao na kadhalika, zote zikitujia kwa pamoja, ni kama wote wonaongea lakini hakuna anayesikiliza.  Kwa hiyo mtu anaweza kujisikia mpweke katikati ya kelele zile, hususani akiwa shidani.

Siku hizi, sisi sote tunaona kwamba teknolojia ni kitu cha kawaida.  Karibia watu wote wanashika simu janja mkononi.  Tunatuma ujumbe, tunapokea barua pepe, tunapiga simu, tunatumia WhatsApp na Facebook.  Tunatumia WeChat, Telegram, yaani kuna njia nyingi ya mawasiliano … lakini je!  Kuna mtu awaye yote anayesikilikza kwa kumaanisha?

Alexander Graham Bell alizaliwa Scotland mwaka wa 1847.  Kama wengi wetu wanavyojua, yeye na mwenzake Thomas Watson walibuni na kutengeneza simu ya kwanza.  Mwaka wa 1915, Bell alipiga simu mara ya kwanza kupita bara zima kutoka jiji la New York akimpigia Watson huko San Fransisco.

Ebu fikiria alivyochangamka wakati alianza kuingiza namba?  Je!  wito wangu utasikika maili elfu mbili na nusu huko?  Je!  Watson ataitika?  Je ataweza kunisikia?

Mara nyingi ni kama Mungu yu mbali sana nasi.  Yamkini yuko bizi sana; labda ana shughuli nyingi.  Nikimwita, je!  Atapokea?  Je!  Atakuwa tayari kunisikiliza?  Je!  Atanijibu?

Zaburi 86:6,7  Ee BWANA, uyasikie maombi yangu; uisikilize sauti ya dua zangu.  Siku ya mateso yangu nitakuita, kwa maana utaniitikia.

Rafiki yangu, Mungu daima yupo akiwa tayari kusikiliza na kupokea ombi lako la kupewa neema, Daima yu tayari siku ya taabu yako kukusikiliza na kukuitikia wakati unamwita.  Daima yuko hivi.  Usiisahau kamwe. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy