Je! Umefungua Karatasi ya Kufungia Zawadi Yako?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Matendo 2:38,39 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
Je! Umefungua Karatasi ya Kufungia Zawadi Yako?
Download audio file
Ebu fikiria ingekuaje kama siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwako, tuseme miaka 20, 30 au 40, yule ambaye anakupenda zaidi anakupa zawadi iliyofungwa vizuri kwa mapambo ya kupendeza. Safi kabisa! Unaguswa sana hadi kutoa machozi. Sasa utafanyaje? Je! Utaiweka bado imefungwa ndani ya kabati na kuisahau kabisa? Isingeeleweka hata kidogo.
Lakini kumbe! Ndivyo Wakristo wengi wanavyoifanyia zawadi ile ya Roho Mtakatifu. Wanaiweka tu. Kwa nini tunafanya hivyo?
Matendo 2:38,39 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
Kwa nini tuko hivi? Labda ni kwa sababu hatutaki kubadilisha mioyo yetu na jinsi tunavyoishi. Labda hatujafahamu Roho Mtakatifu ni nani. Labda tunahofia uwezo wa Mungu kukaa ndani yetu kwa njia ya Roho yake. Au labda … hatujali na hatufikiria habari hiyo.
Nisikilize. Kama umemwamini Yesu, jua kwamba amekusudia kubadilisha maisha yako kabisa na kukuweka huru na dhambi iliyokufunga. Anataka kukusamehe na kukuwezesha uishi maisha mapya. Maisha ya mmojawapo wa watoto wake.
Na kama unampokea Yesu kuwa Mwokozi, kama unakusudia kubadilisha moyo wako na maisha yako kwa ajili yake … ndipo atakusamehe. Ndipo atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu.
Usidanganyike, zawadi hii ni kwa ajili yako. Ifungue sasa … kwa ajili ya Kristo!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.