... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Je! Umewahi Kujiuliza, Kwa Nini …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 51:11,12 Usinitenge na uso wako, wala roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; unitegemeze kwa roho ya wepesi.

Listen to the radio broadcast of

Je! Umewahi Kujiuliza, Kwa Nini …


Download audio file

Hivi umewahi kujiuliza mara kwa mara ni kwanini furaha uliyokuwa nayo, furaha unayoamini kwamba Mungu anataka uwe nayo, imetoweka?…Ni kama Mungu amekuacha!.

Angalia, kuna wakati Mungu anarudi nyuma kidogo ili atupe fursa ya kuzoea kidogo upweke kana kwamba tuko jangwani. Hapo ndipo tabia zetu zinapimwa na kutengenezwa vizuri.  Na jinsi tulivyo sasa, kwa sehemu kubwa ni kwasababu Mungu ametupitisha katika mazingira kama hayo.  Ni fursa kweli.

Lakini wakati mwingine ni kwasababu sisi wenyewe tumeleta utengano huo kwa mwenendo wetu usiofaa; yaani uasi wetu.  Ndio, Mungu bado anatupenda na yuko tayari kutusamehe, lakini ule ushirikiano wa karibu tuliokuwanao umekatika kwasababu pande mmoja umekosa upande wa pili, hapo lazima upande uliobaki uvurugike.

Kujua kwamba umemkosea Mungu hakufurahishi hata kidogo kwasababu furaha uliyokuwa nayo katika ushirikiano wenu umetoweka tayari.  Lakini wewe unajisikia kwamba yeye ndiye aliyekuacha kabisa.

Na hii ilikusudiwa iwe hivyo palei tunapomwasi Mungu.  Yaani imepangwa hivyo ili tuweze kujirudi mapema kutokana na hamu tuliyonayo ya kujua tena furaha ya wokovu wetu.

Ndio maana, Mfalme Daudi, baada ya kuzini na kuua mtu (nadhani hakuna dhambi mbaya kuliko hizo mbili!), yeye aliweza kuomba dua ifuatayo:

Zaburi 51:11,12  Usinitenge na uso wako, wala roho yako mtakatifu usiniondolee.  Unirudishie furaha ya wokovu wako; unitegemeze kwa roho ya wepesi.

Nakusihi, jipe fadhili hii.  unapojua kwamba umeasi, pindi tu unapofahamu kwamba umekosea, jirudi haraka halafu umruhusu Mungu kukujaza na uwepo wake, yaani Roho yake, na kukurejeshea furaha ya wokovu wako.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.