Je! Unafurahia Matembezi?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Ufunuo 3:3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.
Matembezi kwenye meli za fahari yamekuwa chaguo la kwanza kwa ajili ya likizo kwa watu wengi. Kwa kweli, mwaka jana watu zaidi ya miliyoni 30 walifanya matembezi, na baada ya miaka mingine mitatu wanakisia kwamba watafika miliyoni 40 kwa mwaka!
Siku za hivi karibuni, niliona na kusoma menyu ya chakula ya daraja la kwanza kwenye meli ya RMS Titanic historia ya mwaka 1912. Chaza, supu nyepesi, steki, mtoto wa bata aliyeokwa pamoja na sosi ya apple … vyote vikisindikizwa na divai bora iliyotoka Ufaransa, watu walipata huduma ya kifahari sana.
Lakini Meli ile ilivunjika pande mbili na kuzama kilindini futi 12,500 chini ya bahari.
Watu waliokuwa ndani ya daraja la kwanza walikuwa wanaishi maisha bora sana ndani ya meli iliyodhaniwa kuwa haiwezi kuzama, walakini ghafla, kama mwizi ajavyo usiku, barafu ile iliweza kunyanganya uhai wa watu zaidi ya 1,500.
Ufunuo 3:3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.
Haijalishi maisha yanavyopendeza na kuonekana kwamba ni salama katika ustawi, mwisho wa maisha yako, mwisho wa maisha yangu, unaweza kuja ghafla kama hivi. Je! Uko tayari?
Amka. Weka imani yako ndani ya Yesu aliyekufa na kufufuka kwa ajili yako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.