... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Jinsi ya Kumheshimu Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 6:19,20 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Listen to the radio broadcast of

Jinsi ya Kumheshimu Mungu


Download audio file

Siku hizi, wanadamu wanatendea miili yao mambo ya ajabu.  Wanatoboa viungo vyao sehemu isiyoeleweka, wanachora miili yao, wanaipamba, wanaikoga na kuiachilia mambo machafu.  Ni kipi kinachoendelea hapo?

Labda utaniambia, Berni, subiri kwanza.  Mimi nina chanjo kwenye mwili wangu.  Je!  Unasema kwamba ni kosa?  Nimetoboa masikio yangu, je! Ni kosa kweli?  Napenda kuonekana kuwa napendeza, hii haiwezi kuwa kosa.  Sawa.  Lakini kwa mfano, nilisikia mhubiri maarufu akitamka baada ya kupata operasheni ya ngozi ya uso, eti, Ni mwili wangu, naweza kuutendea kama ninavyotaka mimi.

Lakini swali langu ni hili.  Kama wewe ni Mkristo, na una shauku kwa kumfuata Yesu … je!  Mwili wako ni wa kwako kabisa?

1 Wakorintho 6:19,20  Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu?  Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani.  Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Mtume Paulo aliandika maneno hayo akishauri kanisa la Korintho kuhusu zinaa.  Hoja yake?  Mwili wako si mali yako kwa sababu, kama umeamua kumfuata Yesu na kama umepokea karama yake ya huruma na neema, msamaha pamoja na uzima wa milele, basi umenunuliwa kutoka utumwa wa dhambi kwa bei kubwa sana, yaani kifo cha Yesu, Mwana wa Mungu, pale msalabani.

Lengo langu leo si kuhukumu mtu awaye wote kuhusu chanjo lake au kutobolewa masikio au lo lote lile.  Ninachokilenga ni hiki:  Wakati unataka kuamua kuufanyia mwili wako kitu fulani, kumbuka, si mali yako.  Umenunuliwa kwa thamani, kwa hiyo umtukuze Mungu katika mwili wako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy