... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Jinsi ya Kusafiri kwa Wepesi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 12:1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.

Listen to the radio broadcast of

Jinsi ya Kusafiri kwa Wepesi


Download audio file

Kuna sababu wale wanaofaulu katika mashindano ya wanariadha wanapata ushindi.  Ni kwamba hawabebi uzito uzidiyo.  Kama wangiubeba, wasingaliweza kushindina vizuri, wasingekuwa washindi kamwe.

Hii inaeleweka vizuri.  Lakini wakati tunawaangalia wale wanariadha wakikimbia mbio ya mita 100 au wakistahimili mashindano ya marathon ya kukimbia kilomita 42, hili wazo la wao kutokubeba mzigo wo wote haliingii kichwani, tunashuhudia wepesi wao tu.

Kila mtu lazima ashindane kwa kupiga mbio, hata wewe na mimi lazima tukimbie.  Siku moja tutafikia mwisho wa mashindano yetu hapa duniani.  Lakini kumbe!  Watu wengi wanaamua kukimbia wakibeba mizigo mingi; mizigo inayosababisha wakimbie pole pole hata kujikwaa.

Waebrania 12:1  Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.

Kilichowekwa machoni petu hapo ni mfano wa mwanariadha akishindana mbele ya umati mkubwa wa watu.  Ni kazi ngumu; haikukusidiwa kamwe kuwa rahisi.  Kama ni vigumu hivi, kwa nini sasa kujikwamisha kwa kubeba mzigo uzidio wa dhambi, dhambi inayotuzinga?  Haieleweki kabisa.

Watu wa Mungu wengi wanatamani “kuenenda katika Roho” na kuwa na uhususiano na Yesu unaoridhisha.  Ni vizuri sana.  Lakini wajue ya kwamba hatua ya kwanza ni hii:  Kuweka kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi.  

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy