Jinsi ya Kushinda Fadhaa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yoshua 1:9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako yu pamoja nawe kila uendako.
Wakati hali ya mambo yanayotukusanyikia kama dhoruba ya kutuangamiza, ni kama hisia zetu na zenyewe zinayaunga mkono na kufanya hali kuwa mbaya zaidi. Sijui kama umeshaona hayo?
Ni kama Mungu alitaka kunipima leo asubuhi. Wakati nilikuwa ninaandaa ujumbe huu, ghafla nilijikuta ninakabiliana na ishu ngumu mno ambayo ingeathiri huduma yetu. Na hata wewe, hisia zangu hazikunisaidia, bali zilizidi kunivuruga.
Mimi ni kiongozi hapa. Mimi ni mwenye kutegemewa na watu wakati mambo yanakuwa magumu. Lazima niwe yule ambaye imani yake haitetereki pamoja na kuwa naweza kusngwa pia.
Yoshua 1:9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako yu pamoja nawe kila uendako.
Hilo ndilo lilikuwa neno ambalo lilimjia Yoshua, baada ya kifo cha Musa, wakati ilimbidi achukue nafasi ya kuwa kiongozi wa Israeli na kuwaongoza vitani na kupambana hatua kwa hatua.
Ilikuwa kipindi kinachotisha kweli, na wakati mtu anatishiwa, kuna hisia mbili zinazojaribu kumtawala. Ni hofu na fadhaa. Lakini fadhaa – yaani hisia kwamba tumeharibikiwa mno wakati mambo hayaendi kama tulivyotazamia
Kama unakabiliana na hali hiyo, nisikilize. Uwe hodari na moyo wa ushujaa. Unajua kwa nini?
Kwa kuwa BWANA, Mungu wako yu pamoja nawe kila uendako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.