... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Jinsi ya Kutambua Uongo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 86:11 Ee BWANA, unifundishe njia yako; nitakwenda katika kweli yako; moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako.

Listen to the radio broadcast of

Jinsi ya Kutambua Uongo


Download audio file

Ukitafakari kidogo, mtu anaweza kutambua kwamba njia fulani hainyooki, kwa sababu anaweza kuilinganisha na njia iliyonyooka.  Lakini ili aweze kulinganisha, lazima ajue vizuri njia iliyonyooka inafananaje.

Vivyo hivyo, kama hujui ukweli, utashindwa kutambua uongo.  Kinachohuzunisha ni kwamba watu wengi zaidi wanadanganywa na uongo. Mfano, wa uongo kwamba mali inamletea mtu furaha umesababisha maumivu mengi.  Uongo kwamba hisia zetu lazima zitawale ukweli, ni uongo unaopotosha wengi.

Yaani, tungeweza kuorodhesha mifano mingi tu

Swali ni:  Je!  Mtu atawezaje kutambua uongo huu wa kishetani na kubaini?  Tunawezaje kuwekwa huru na uharibifu ambao daima unaletwa na huo uongo?  Jibu …

Zaburi 86:11  Ee BWANA, unifundishe njia yako; nitakwenda katika kweli yako; moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako.

Ni kumkabidhi Mungu shauku zote za mioyo yetu.  Ni kumwomba atufundishe njia yake na kutuongoza ndani yake ili tuweze kutembea katika kweli yenye umuhimu, yaani kweli yake Mungu.

Ni kumwomba atengeneze mioyo yetu ili tupate ushindi katika mvutano uliomo kati ya mema na mabaya

Ee BWANA, unifundishe njia yako; nitakwenda katika kweli yako; moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy