Jinsi ya Kuwa na Nguvu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 30:15-17 Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali. Bali ninyi mlisema, La! Maana tutakimbia juu ya farasi; basi, ni kweli, mtakimbia; tena, Sisi tutakimbia juu ya wanyama waendao upesi; basi, wale watakaowafuatia watakuwa wepesi. Elfu moja watakimbia kwa kukemewa na mtu mmoja; kwa kukemewa na watano mtakimbia; hata mtakapoachwa kama mlingoti juu ya kilele cha mlima, na kama bendera juu ya kilima.
Ni kweli kinzani kwamba wakati tunahitaji nguvu zaidi, ni pale tunapojisikia kuwa wadhaifu kabisa. Ni wakati nguvu zimetuishia, ndipo tunayozihitaji zaidi. Yaani, inasumbua kweli!
Wakati mambo yako shwari, hatuna haja kuongezewa nguvu. Hamna sababu. Lakini hapo ndipo tunapoweza kudanganywa kana kwamba tuko salama wakati huko mbeleni kuna hatari. Sasa hatari ile ikitujia ghafla na tukipambana nayo, mara moja kujiamini kwetu tuliokuwa nako, kunatoweka.
Hapo ndipo inambidi mtu kufanya maamuzi. Au atamgeukia Mungu amevushe kipindi kile kigumu, ao atategemea nguvu za kibinadamu. Na kama tunaenda kugundua, chaguo lililo sahihi, na la muhimu sana.
Isaya 30:15-17 Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali. Bali ninyi mlisema, La! Maana tutakimbia juu ya farasi; basi, ni kweli, mtakimbia; tena, Sisi tutakimbia juu ya wanyama waendao upesi; basi, wale watakaowafuatia watakuwa wepesi. Elfu moja watakimbia kwa kukemewa na mtu mmoja; kwa kukemewa na watano mtakimbia; hata mtakapoachwa kama mlingoti juu ya kilele cha mlima, na kama bendera juu ya kilima.
Unaona utofauti kati ya maamuzi hayo mawili – ama kumtegemea Mungu ama kuitegemea nguvu ya kibinadamu – yaani yako kinyume kabisa. Kuna njia moja tu kuendelea kuwa na nguvu. Ni kumwendea Mungu, ni kutulia na kumtumaini, basi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.