Jitakase Nafsi Yako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Wakorintho 7:1 Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.
Mungu hua ameahidi ahadi kubwa mno kwa wale ambao wamemwamini Yesu. Ameahidi kwamba atakuwa Mungu wetu, na sisi tutakuwa watu wake; kwamba ataishi katikati yetu. Ahadi hizo zimetokana na shauku kubwa aliyo nayo ya kutukaribia.
Ni jambo jema kulijua. Wakati umeanguka chare, wakati unajisikia kwamba uko peke yako, wakati unafikiri kwamba hakuna anayekuelewa … kujua kwamba Mungu ana shauku ya kukukaribia ni jambo la ajabu mno. Ni faraja kubwa sana!
Sasa, mtu angeitikiaje ahadi hiyo? Mtu angeishije ili aweza kuiheshimu na kutegemea ahadi hiyo? Mtume Paulo alijibu swali hilo wakati aliandikia kanisa la Korintho:
2 Wakorintho 7:1 Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.
Utakatifu ni kitu ambacho sisi sote tunakitamani. Dhahabu safi. Upendo safi. Kujitolea kikamilifu. Uhalisi na kutokuwa na unafiki unaotokana na usafi unatuvutia, wewe na mimi … na hata Mungu pia. Tungeishije? Tungeitikiaje upendo wa Mungu? Kwa kujiepusha na lo lote ambalo lingechafua miili yetu na nafsi zetu.
Je! Utaniruhusu leo nikikuuliza moja kwa moja, je! Unacho kitu gani katika fikra zako, matamanio yako, matendo yako ambacho unajua hakika kwamba kinachafua ule utakaso Mungu anatamani kuona ndani yako? Kwa moyo wangu wote, ninakusihi, kitoe kabisa. Kwa sababu inabidi tutimize utakatifu wote katika kumcha Mungu. Utakaso.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.