Katika Matatizo Yetu Yote
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 5:3-5 Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.
Leo hii, kama ungeandika kwa karatasi mambo yote ambayo ungependelea yasiwepo maishani mwako, mambo ambayo ungetamani uwe na uwezo wa kuyafuta moja kwa moja, orodha hiyo ingeonekanaje?
Hakuna mtu angekosa kutaja mambo fulani, si kweli? Labda ni mambo madogo-madogo yanayokusumbua, au labda ni jambo moja au mawili makubwa yanayokuharibia maisha.
Haijalishi ni mambo gani, lazima yakuibie amani na furaha na kusababisha usifurahie maisha. Sasa, kwa kuwa Krismas imekaribia sana, labda unabaki kwa kujiuliza, Nitawezaje kusherehekea sikukuu nikiwa katika hali kama hii?
Jana tuliona jinsi Mtume Paulo alifurahi pamoja na rafiki zake Rumi, kwa sababu ya mibaraka ya ajabu inayotokana na imani kwa Yesu. Yaani amani, neema, baraka, furaha, tumaini, utukufu. Mambo yaliyo bora kabisa! Lakini mara moja anaongeza maneno yafuatayo:
Warumi 5:3-5 Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.
Rafiki yangu ujue haya. Yesu yu pamoja nawe katika shida zako, katikati ya matatizo uliyo nayo, pia amekukaribia zaidi ili akusaidie. Tunajuaje kwamba hii ni kweli? Ni kwa sababu pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. Shikilia ukweli huo. Kwa sababu …
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.