... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kiasi na Saburi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Petro 1:3,5,6 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe ... Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi.

Listen to the radio broadcast of

Kiasi na Saburi


Download audio file

Nafikiri sisi sote tunaelewa jinsi mtu anaweza kushindwa kuendelea kuvumilia.  Mfano, wakati mtu anasumbuliwa na kupitia kipindi kigumu… mtu anaweza kuanza kuchanganikiwa na kusikia jazba inapanda ndani yake.  Sisi sote tumewahi kupitia hali kama hiyo.

Ninakiri kwamba mimi ni mtu ambaye anataka mambo yote yakamilike, lakini ninajitahidi kuachana na mtazamo huo kwa sababu hakuna kilichokamilika asilimia mia.

Kwa kweli, kama tumeshaona hizi siku chache, Mungu ametukirimia uwezo wote unaohitajika kuishi maisha ya utauwa.  Lakini ni dhairi kwamba inatubidi sisi tushirikiane naye katika utekelezaji wa baraka hizo.

2 Petro 1:3,5,6  Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe … Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi.

kiasi ni sehemu ya tunda la Roho Mtakatifu kama vile saburi ilivyo.  Sasa ukitafakari kidogo, utaona kwamba saburi ni kuendelea kuwa na kiasi kwa muda mrefu.  hii ni kweli kabisa.

Lakini siyo rahisi kwangu, kwa hiyo ninafanyaje wakati ninaanza kukasirika?  Ninaomba hivi, Bwana, tafadhali niongezee saburi.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy