Kiburi Huwa Kinaathiri
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 2:5-8 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijenyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Kwa miaka mingi sasa, nimekutana na watu wenye akili, watu ambao wamefanikisha mambo yao kabisa. Sijui wewe? Watu wanaoweza kukamilisha mambo makuu kuliko wewe na mimi. Lakini kuna kitu kimoja ambacho huwa kinaangusha wengi wao.
Ukweli ni kwamba, mtu anaweza kuwa na akili, katili, na akafaulu kabisa pamoja na ukorofi wake. Mtu anaweza kushinda kabisa japo kuna mambo mengine yanamshinda. Yaani ni mchanganyiko unaoshangaza watu mara nyingi.
Ni tanzia kusema ukweli, kwa sababu, kiburi kinamwangusha mtu, watu kama hawa wanaangukaga chali. Niliwahi kumsikia mtu akisema kwamba kiburi kinamnyanganya mtu faida yote ya maadili yake mbele za Mungu, na ningeongezea hili, hata mbele za binadamu wenzake.
Unaweza kuwa mtu mwenye akili kuliko wote duniani, lakini ukiwa mpweke kabisa kwasababu watu wengine (na Mungu pia) wanachukizwa na kiburi chako. Ndio maana ni muhimu sana kuondoa kiburi moyoni mwako kabla hakijakuathiri, kwasababu kwa vyovyote kitakuathiri. Daima kiburi kinatangulia anguko. Halafu njia bora ya kuseta kiburi ni ipi?
Wafilipi 2:5-8 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijenyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Lakujikumbusha: Njia bora ya kuseta kiburi ni kumfuata Yesu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.